Waziri Mkuu Majaliwa amezungumza na Balozi wa Marekani Dkt. Donald J. Wright.

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa leo Juni 16, 2022 amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Marekani Nchini Tanzania Dkt. Donald J. Wright katika Ofisi ndogo za Waziri Mkuu zilizopo Magogoni jijini Dar es Salaam. Waziri Mkuu na Balozi Wright wamezungumzia namna nzuri ya kuimarisha ushirikiano mzuri uliopo kati ya nchi hizo mbili katika Sekta za